Friday, November 2, 2012

TEMBA NAYE AIBIWA VIFAA KWENYE GARI LAKE


Alfajiri ya kuamkia leo, Mh Temba ameibiwa vifaa vya  gari lake aina ya verossa akiwa amelipaki nyumbani kwake.Temba amesema vifaa vilivyoibiwa ni pamoja na power window, side mirror zote taa za nyuma, radio leseni,na vinginevyo ambavyo thamani yake hajaijua kwa sasa.

"jamaa siwajui ila wamekuja na wameniibia power window, taa za nyuma, sidemirror vitu vya ndani wameiba radio, leseni hadi madaftari yangu ya shule, makaratasi, sasa sijui atakua ametumwa au anafanya maksudi yaani anaiba mpaka madaftari" amesema temba

lakini baada ya wizi huo temba alipiga simu polisi na kati ya info alizopewa na washkaji zake walio central si unajua jamaa likua mwanajeshi kitambo sasa baada ya kuongea na watu wa usalama alipewa ripoti kuwa kuna watu wameamua kuwakomoa wasanii pamoja na watangazaji, kwa kuwaibia mpaka mwenzao alieshikiliwa aachiwe

" kituoni sasa hivi mishe mishe zilizokuwepo ni kwamba kuna jamaa wametangaza kwamba wanaibia wasanii wote magari na mapresenter nao watakoma mpaka mtu wao wakaribu aachiwe, naskia kuna mtu wao ambae wanafanya nae kazi amekamatwa yuko ndani wamesema kwamba wataibiwa wasanii wote na vitu vya magari kwasababu ndio wamesababisha mtu wao amewekwa ndani..." amesema temba

weekend iliyipiya msanii Suma lee aliibiwa gari lake aina ya Land cruser VX yenye thamani ya shilingi milioni 70 maeneo ya coco beach alipokuwa amelipaki na mpaka leo hii halijapatikana tukio lililotokea wiki kadhaa baada ya gari la Ommy Dimpoz kuibiwa vifaa pia

Temba alimalizia kwa kusema, kama angepata nafasi ya kuwakamata wezi hao basi angewatembezea kvipara raaaaaah

zaidi msikilize temba hapo chini

Sunday, October 7, 2012

NAMRUDISHA KWAO | KIMBUNGA,ROMA,JOSE MTAMBO & DOMOKAYA

NAMRUDISHA KWAO | KIMBUNGA,ROMA,JOSE MTAMBO & DOMOKAYA

BIFU LA ANTI-VIRUS NA CLOUDS MEDIA GROUP LAMGEUKIA CYRILL

Bifu kati ya kundi la Anti-Virus (Vinega) linaloongozwa na Mhe. Joseph Mbilinyi aka Sugu, mbunge wa mbeya mjini na Clouds Media Group chini ya Ruge Mutahaba limegeukia kwa Cyrill Kamikaze baada ya Cyrill kuwapa Clouds msemo wa 'bhaaaaaas' kutumika katika Serengeti Fiesta 2012.                       Msemo huo ulipelekea kundi pinzani la Clouds Media Group yaana Anti-Virus kuona kuwa cyrill anajipendekeza kwenye kampuni hiyo ya vyombo vya habari hivyo. Ambapo PeenLawyer toka kundi la Anti-Virus alimshushia Cyrill matusi na kudai kuwa tayari wameandaa 'mix tape' kwa ajili ya kumchana Cyrill kwa suala alilolifanya. Akizungumza na 'Tripple B' ya Nyemo Fm siku ya jumamosi tarehe 6 Octoba, mwaka huu, Cyrill ameeleza kuwa tayari amesikia na kuona habari ya PeenLawyer wa Anti-Virus kumtukana yeye Cyrill toka kundi la WAKACHA katika mitandao na media mbalimbali lakini yeye hajari kwani anawafananisha wao na watu wenye ufinyu wa mawazo. Aidha msanii huyo toka Wakacha ameendelea kusema kuwa mwanzo aliona Anti-Virus ni kundi linalotetea haki za wasanii lakini kwa sasa anawaona kama wanafiki tu na hana habari nao tena, kwani matusi alioyapata toka kwa PeenLawyer kwa kuambiwa kuwa yeye ni kama condom inayotumika kujikinga na magonjwa kama gono na matusi mengine ya mama imemuma sana lakini ameamua kuwaacha kama walivyo. "Msemo wa bhaaaaas ni msemo niliokuwa nikiutumia mimi pamoja na kundi langu ambapo wana-clouds waliomba utumike katika Serengeti Fiesta 2012, sasa nashangaa wao wanavyonitusi mimi kwa sababu ya bifu lao" Alisema Cyrill Kamikaze kwenye interview ya 'Tripple B' ya Nyemo Fm.

Friday, September 14, 2012

JAY-Z KUCHANGISHA KWA AJILI YA KAMPENI ZA OBAMA

Ushikaji wa Jay-Z na Barrack Obama rais wa Marekani utaendelea wiki ijayo, pale rapper huyo na mkewe Beyonce Knowles watakapoendesha shughuli ya kuchanisha fedha kwenye `Fundraising dinner` katika klabu ya Jay,40/40 ya Manhattan.Dinner hiyo wataalikwa watu 100 ambapo kila moja atalipa dola 40000 kwa ticket. gazeti la NEW YORK POST limeeleza kuwa dinner hiyo ya sept. 18, inadaiwa kuwa kituo cha mwisho kampeni ya Obama jijini New York kabla ya uchaguzi.

FA aamua kufuata nyayo za AY

Rapper Mwinjuma Hamis aka Mwana FA, ameamua kufuata nyayo za swaiba wake AY kutaka kufanya video kali za gharama kama anazofanya AY. Japo hatofanya video ya dola 20,000  kama `party zone` ya AY. Mwana FA anatarajia kukata dola 8,000 kumlipa director tu wa video yake na hiyo haijumuishi gharama zingine. Aidha FA ameongeza kusema kuwa video atakayoifanya ni ya wimbo wake mpya aliowashirikisha WYRE na PREZZO alioupa jina la `Give me that song` uliofanyika nchini Kenya. Video hiyo itafanyika Nairobi, Kenya japo hakutaja kampuni ama director atakayehusika.

GQUICK ROCKER KUFUNGUA RECORDING STUDIO

Msanii wa kundi la Rockers, Abbott Charles aka Quick Rocker amesema anaanzisha record label yake aliyoipa jina la 255. Rapper huyo anayetamba na ` club banger` yake mpya inayoitwa  `katika` alisema pia anafungua studio yake ya kurekodi muziki  aliyoipa jina BIG STEP. Aidha hitmaker huyo wa BULLET ameongeza kusema kuwa pamoja na kuwa pamoja na kuwa na studio yake, bado hataacha kufanya kazi na studio zingine na producers tofauti tofauti  ili mradi apate kitu kizuri.